Kusindika Mazao
Tanzania inajulikana sana kwa uzalishaji wa mazao ya kuuza nje ya nchi yanatotokana na sekta ya kilimo. Mazao hayo ni kama mahindi, kahawa, pamba, Mkonge, Ufuta, Alizeti, chai, matunda nk. Sekta ya kilimo sio tu kwamba inaongoza kwatka uzalishaji kwenye uchumi wa Tanzania bali pia njia ya kujipatia riziki kwa watu wengi wa Kitanzania. Sekta hiyo inajumuisha uzalishaji wa mazao ya viwandani na chakula, na kuendesha sekta zingine kama, mifugo, uvuvi.
Uzalishaji katika sekta ya misitu na mazao na kilimo cha bustani huchangia asilimia 29 ya pato la taifa la kilimo, wizara ya fedha nchini Tanzania ina taasisi nyingi ambazo zinatoa msaada maalum wa kifedha kwa biashara zinazozingatia kuongeza thamani mazao yanayotokana na kilimo, ikiwemo benki ya maendeleo ya kilimo
Kilimo huchangia karibu 85% ya mauzo yote ya nje, na kimeajiri angalau 80% ya watanzania. Kuna zaidi ya hekta milioni 44 za ardhi inayolimwa inayopatikana Tanzania, na hekta milioni 29.4 zinafaa kwa umwagiliaji. Kilimo kina jukumu kubwa katika ukuaji wa viwanda nchini, ikitoa uwezekano wa kutoa masoko ya bidhaa za viwandani na malighafi kwa viwanda. Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi inayolimwa na wastani wa hekta milioni 29.4 zinazofaa kwa umwagiliaji.
Tanzania inakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, kushiriki katika uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo kupitia program za EPZ na SEZ, ambazo zimeweka ili kuhusumia wawekezaji na kuwapatia vivutio mbalimbali vya kibiashara na kiutendaji.
Fursa Zilizopo ni Pamoja na:
- Kufanya kilimo kikubwa cha biashara ya mazao kama vile miwa, mchele, ngano, kahawa, chai, alizeti, kunde, kilimo cha maua, pamba, mkonge, zabibu, simsim na mahindi.
- Uwezo mkubwa wa kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari. Kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari huungwa mkono na vyanzo vingi vya maji, hali nzuri ya hali ya hewa na uwezo mkubwa wa soko
- Uwezo mkubwa katika uwekezaji katika Viwanda vya Kilimo na Usindikaji wa Kilimo
- Maendeleo ya wakulima wa kawaida kusaidia vyanzo vya malighafi kwa viwanda kama inafaa
- Upanuzi na uboreshaji wa mifumo ya umwagiliaji; uboreshaji wa R&D katika kilimo cha mazao

