Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje

Mamlaka ya  Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje

Viwanda vya kujitegemea - EPZ

Viwanda vya Kujitegemea chini ya lesini ya EPZ

Katika sheria ya EPZ ya mwaka 2002, pia yenye marekebisho mwaka 2006, inaruhusu watu binafsi kuwa na mweneo ya EPZ kwa maana ya kuwa na kiwanda ambacho kinazalisha bidhaa kwaajili ya kuuza nje ya nchi. Kupitia program hii, makampuni mengi zaidi yanaendelea kufanya uzalishaji kwaajili ya mauzo ya nje katika maeneo mbalimbali ya tanzania bara. faida ya program hii ni kwamba mtu anaweza kujenga kiwanda chake popote Tanzania bara, kwenye eneo analolipenda na linalomfaa mradi wa uwekezaji wake na kupata vivutio vyote kama wawekezaji ambao wako katika maeneo ya SEZ.