News

Posted On: Jan, 14 2019

DAWASA yaagizwa kupanda miti Laki Moja

News Images

Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa ameagiza DAWASA kupanda miti laki moja katika vyanzo vya Maji ilikulinda mazingira ya vyanzo hivyo . Hayo alisema katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika katika wilayani Bagamoyo Januari, 2019 .

"Nilazima DAWASA Mpande miti laki moja kwa kipindi cha mwaka huu mmoja ilikulinda vyanzo maji kwa kuwa uharibifu wa vyanzo usababisha kuongeza gharama za uzalishaji" alisema Prof. Mbarawa.

Aidha Prof. Mbarawa amewataka watumishi wa DAWASA kufanya kazi kwa bidii kwa kutoa huduma bora ilikuongeza makusanyo ya taasisi kufikia bilioni 12 na kuboresha mishahara wafanyakazi.

kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amemshukuru waziri wa Maji kushiriki katika zoezi la upandaji miti nakuhaidi kufikia makusanyo ya bilioni 12 kama wizara ilivyoagiza.